Hisa Bank
Ushauri
Kanunue hisa za crdb ambazo zinauzwa at shs 420 per share. 10 m itakupatia shares 23,809. Lakini ukinunua shares hizi crdb ukakaa nazo baadae ukazipeleka kwenye soko la hisa unaweza ukaziuza zote halafu ukavuna zaidi ya asimia 100. Na hii ni baada sana sana ya miezi kadhaa au mwaka. Kwa hiyo ukipata 20m zako iko mbaya gani/ U can decide kuziweka kwenye Fixed deposit ya hao crdb halafu ukaitumia hiyo kuombea mkopo. But this depends very much if u have a steady monthly income. Huo ni ushauri wangu wa bure
Haya mambo ya stock market wadau wanasema sometimes huwa yanakuwa pata potea. Kwa jinsi ulivyoweka maelezo yako, it is like unauhakika kuwa bei za hisa zitapanda huko mbeleni which is a fallacy.
Stock market are stochastic in nature na kuna factor nyingi mno zinzaochangia bei kushuka au kupanda. Some of the factors are internal and can be internally controlled, some are external and never be controlled. Ni vyema mhusika asichukulia maneno yako in totality.
Ufugaji
Ufugaji wa ngombe kwa mchakato ufuatao:
Ujenzi wa banda = Ths 500,000/=
Manunuzi ya Ngombe 5 x Tsh 900,000 = Tsh 4,500,000/= (Ngombe utawanunua wakiwa na mimba ya miezi 6)
Kuwahudumia ng'ombe kwa miezi mitatu kabla ya production = Tsh 1,500,000/= (inahusisha mshahara kwa wafanyakazi wawil + chakula + madawa)
Jumla = Tsh 6,500,000/=
Baada ya Miezi 3;
UZALISHAJI: Ngombe hawa watakuwa wakitoa maziwa si pungufu ya lita 5 kwa asubuhi na jioni kwa kila ng'ombe. Hivyo uzalishaji kwa siku utakuwa lita 10 kwa siku kwa ng'ombe.
MAPATO
Lita 10 x Ng'ombe 5 = lita 50 kwa siku x Tsh 1500 (bei ya kuuzia sehemu mbalimbali) = Tsh 65,000 kwa siku Mapato kwa mwezi = Tsh 65,000 x 30 = 1,950,000/= Gharama za uendeshaji kwa mwezi = Tsh 900,000/=
Faida = Tsh 1,050,000/= kwa mwezi.
BAADA YA MIAKA 5:
Kumbuka ng'ombe huzaa kila mwaka hivyo basi baada ya miaka mitano utakuwa na ng'ombe wasiopungua 25. Kipato chako kwa mwezi unaweza kufikia si pungufu Tsh 4,200,000 endapo utakuwa na ngombe jike 20 kati ya hao 25.
Kuchukua tenda ya supplier
Unaweza kufungua kampuni na kazi yako kubwa ikawa kusambaza bidhaa na huduma mbalimbali zinazohitajika maofisini na sehemu mbalimbali.
Ni kweli kazi hii inalipa sana lakini upataji kazi wake ni mgumu sana. Unatakiwa kuwa na network ya uhakika. Pia kwa supplies hiyo pesa ni ndogo kwani unaweza pata kazi ya kwanza ukatakiwa utumie say 15m na malipo yakaje say 3 weeks after say 3 weeks. Kwa namna hiyo kama huna 'rescue plane' yaani mtu wakukupa pesa kiasi chochote unachotaka muda wowote itakushinda. Mdau mmoja alifanya ila changamoto aliyokuwa akikumbana nayo ilikuwa kupata kazi kwani alikuwa na rescue plane anytime akitaka pesa anaonyesha LPO jamaa fasta anamwezesha. Kwa kuongezea ushauri unaweza kwenda kukodi heka kadhaa Dodoma ulime Zabibu soko guaranteed na Breweries mkuu.
Visima Vya Maji
Unaweza kuwekeza kwenye mfumo wa maji safi kule vijijini, kwa kwenda sehemu ambazo hawana maji ya bomba na ukachimbe visima vya kutumia mota ya umeme ili wapate maji safi badala ya kuchota maji kwenye madimbwi. Hiyo pesa unaweza kuchimba visima 3, hapo utasaidia wananchi wenzako. Unaweza kurudisha pesa yako, iwapo utafanya kila ndoo ya maji ni shs 200.
CHOO CHA KULIPIA
Ukiweza kupata vile vyoo vya kuhamishika ndio vizuri zaidi na unakuwa unaviweka sehemu zenye mkusanyiko wa watu wengi eg. Kariakoo, Mwenge, Tegeta sokoni, Bunju sokoni. Utakuwa na uhakika wa kurejesha gharama zako ndani ya muda mfupi kama ifuatavyo:
Wateja
- Akina mama (200 * 100/= * 30days) = 600,000/= - Akina baba (150 * 100/= * 30days) = 450,000/=
- Watoto/vijana/wanafunzi (200 * 100/= * 30days) = 600,000/=
JUMLA KWA MWEZI 1,650,000/=
Kwa mwaka (19,800,000), kwa miaka kumi (198,800,000/=). Yaani baada ya miaka kumi utakuwa millionea mkubwa sana
NB: Kumbuka, uzuri mmoja kwa biashara hii, haina suala la mvua wala kiangazi. Kila siku biashara inaenda
MITI
Leo niwape item ya tatu tu. Kuna miti mingi ila mizuri ni hii; mitiki(10, nje),milingoti boriti(8),milingoti nguzo (10), milingoti mbao (15),mikrismas(cyprus mbao) (25), pines (12),ktk mabano ni miaka toka kupanda mpaka kuvuna. Soko la mitiki liko nje ya nchi,locally hakuna commercial market mpaka Kilombero wakijenga kiwanda.
Mbegu zinapatikana kwa wakala wa serikali Morogoro, Iringa, Arusha, Tanga etc. Mbegu za mitiki ni ngarambe kuotesha, kilo moja ni Tsh 6500/ na ukifuata utaalam unapata miche 1000 hivi, lakini wajanja wanafanya kienyeji na wanapata zaidi au wanatumia suckers fulani hivi. Bei ya mche kwa sasa ni Tsh 550/ ya chini na 2100/ ya juu pale dar. Pine/cyprus kilo moja ni Tsh 19,500/ na unapata miche 30,000 mpaka 35,000 inatosha eka hamsini ya miti ya mbao.
Mlingoti kilo moja ni Tsh 23,500/ na unapata miche 110,000. Unapanda boriti eka 100 na unapanda miti ya mbao eka 200. Utamu uko ktk boriti. Eka moja ni boriti 1400,bei ya boriti moja kwa leo hii ni Tsh 17,000/shambani.
Kwa hiyo eka moja iliyogharimu Tsh 150,000/ kununua ardhi mpaka kupanda itakupa 1400 x 17,000/=( ) toa gharama za fire break mara moja kwa mwaka. Hakuna kupalilia wala kumwagilia. Mitiki peke yake inakubali pwani,mingine yote ni ktk nchi za baridi.
ARDHI IRINGA. Uzuri wa IR ni huu,ardhi ipo,mvua zinanyesha sana, barabara zipo, wahehe wanaogopa kuiba cha mtu, wahehe hawabagui mgeni. Wewe fanya kilichokupeleka kwa utaratibu basi, halafu unaambiwa karibu tena. Wasichotaka, usiwadharau tu basi. Kazi wanafanya kwa kiwango cha kuridhisha ila baadhi ya vijiji tutapeli tumeingia.
Milingoti hasa Saligna na grandis, ina kuwa haraka na ni multipurpose yaani waweza kuuza kama nguzo za umeme, au boriti za kawaida au ukachana mbao. Wewe ukiwa na milioni moja inatosha kununua eka kumi na kupanda miche 6000 ya milingoti/pines ya mbao, kisha unaondoka kurudi zako mjini. Unakwenda huko june kuweka fireline na kurudi tena mjini. Baada ya miaka mitatu unaprun miti yako. Kwa hiyo mwendo ni huo.
Rafiki yangu na vijana wengine wameunganisha nguvu na kununua eneo kubwa, na kuotesha wenyewe miche ya pines/mlingoti na kupanda ktk plots zao. Mwaka huu wamepanda miti laki tatu kwa pamoja na wako sita tu. Ila mpaka sasa vijana waliopanda miti eneo hilo wako 24 hivi. Msimu ujao watakuwa kama 30 jumla. Wenzao walikwama msimu huu kwa sababu mbalimbali.
Wana jirani mmoja kutoka Kenya yeye peke yake amepanda milingoti milioni nne. Yeye ardhi kapewa na serikali yetu tukufu. Usijali ndo hali halisi. Mmalawi mmoja kajimegea eka 1000 na amepanda miti.
ALIZETI
Mradi mwingine mzuri wa bei nafuu ni mradi wa kukamua alizeti. Mwaka jana nilipata bahati ya kutembelea Singida kwa ziara ya kitume. Nikapata muda nikaenda mitaa ya SIDO. Nilitembelea viwanda vidogo vya kukamulia alizeti. Nikatafiti gharama za mradi wote ule. Kwa mujibu wa Sido,mtambo wenyewe unafikia Tsh 8,000,000/ kwa mwaka jana. Ila mitambo ya mitaani inaweza kuwa chini ya hapo. Gharama za jengo zinategemea sehemu.Ukiweza kufunga kimtambo hicho,mikopo ya upanuzi toka Sido ni mingi bila urasimu. Wale jamaa wanatengeneza hela sio mchezo. Nimegundua pia kuwa watu wanarudi ktk matumizi ya mafuta ya nafaka sana na ukulima wa alizeti/ufuta unaongezeka sana.
GARI
Kwa Tanzania Mil. 10 unaweza kupata faida ya mwaka kama ifuatavyo:
Ukanunua used Corola na kuifanya taxi. Mradi huu unakuhakikishia a minimum net revenue ya Shs 2.92 mil per year (8000*365).
Ukopeshaji
Anzisha ka-saccos kasiko rasmi (zikopeshe at interest): 10 mil * 20% = 2 mil
Mashine ya kufulia
Hostel za wanafunzi wa kike na wa kiume wanaonekana wa wana uwezo mkubwa kidogo wa kujikimu weka mashine zako tatu kila moja 400,000 to 450,000. Zinapatikana mlimani city na baadhi ya mall nyingi kubwa nchini zinapatikana.
Gharama za chumba kupanga tufanye Tshs 80,000 kwa mwezi. Unalipia miezi mitatu, maji, umeme na kufanya kulipa wafanyakazi mishahara ya kawaida..utapiga hesabu..
Total isizidi 5m mtaji mzima mpaka kufungua.
No comments:
Post a Comment