Saturday, January 3, 2015

DAR na PANYA ROAD

Katika jiji lenye kila aina ya huduma na linaloishi viongozi wakuu karibia wote wa nchi tukio kama lililotokea jana la vijana wadogo wa PANYA ROAD. Ni aibu sana kwa kile polisi walichofanya kwa kushindwa kuzuia tukio kabla halijatokea, kutotokea kwenye tukio wakati linaendelea na kukimbia katika vituo vyao vya kazi na kusababisha hata wananchi waliokimbilia katika vituo hivyo kukosa msaada walioutegemea.

Ni wakati sasa wa Rais JK kuamua kuchukua hatua madhubuti kwa kuwawajibisha watu wote hasa wakuu wa TISS na jeshi la polisi kwa kusababisha uzembe ambao umesababisha mali nyingi sana za watu kupotea na pia watu wengi kuumia wakati wa purukshani za kuwakimbia hao wafuasi wa kikundi cha PANYA ROAD.

JK kama Rais licha ya kuonesha udhaifu mkubwa kwenye mambo mengi ya nchi hii toka amekabidhiwa walau ajitahidi kwenye hili la usalama wa raia wake maana kama akiendelea kupuuzia mambo ya msingi kama haya ni kwamba analea makubwa zaidi kutokea ndani ya siku za usoni.

Tuelewe kuwa hawa PANYA ROAD jana hawakuweza kufika sehemu zile za mageti na ulinzi mkubwa kama MASAKI, OYSTERBAY, KISUTU, MBEZI BEACH, UPANGA hili ni kutokana na wao kuwa na silaha na vitendea kazi duni za kuweza kuwafikisha huko na kuwa na uhakika wa usalama wao.

Ila angalizo langu ni kuwa sehemu ambazo hazikufikika jana wasijione kama wao wapo salama kama hali ya serikali yetu na vyombo vya usalama wataendelea tu kusinzia na inteligensia kufanya kazi tu kipindi wanaposikia kuna maandamano ya UKAWA.

Hawa vijana tunaowaacha na kuwaongeza mitaan pasipokuwa na ajira wala kuwa na uhakika hata wao kujua ni wapi wataweza walau kupata mlo wao wa kila siku. Sisi kama taifa tujue kuwa tumeshashindwa kujikamua katika harakati za kusonga mbele.

Rais inampasa kupinga udharimu wote kwa vitendo unaosababisha hali ngumu kwa wananchi wake na faida ya walio wachache vinginevyo vikundi kama PANYA ROAD vitaendelea kuongezeka kila uchwao.

Kitendo cha jana cha vijana wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 18-23 wasiokuwa na mafunzo ya kijeshi kuweza kulidhibiti jiji takribani lote hii ni hatari iwapo maadui zetu wa ndani na nje wakiamua kutumia udhaifu uliopo kwa kuamua kudhamini vikundi vya aina hii kwa kuwapa uwezo wa kifedha, mafunzo na silaha. Nchi hii ambayo tunajivunia kuwa kisiwa na amani na utulivu sifa hii itapotea kabisa.


Moja ya comment ya mdau kwenye mtandao
Makundi ya panya road, mbwa mwitu , watoto wa mbwa na wamarekani weusi ni matokeo ya ufisadi wa muda mrefu unaofugwa na kuenziwa na genge la magamba , ni hivi , kama Anna Tibaijuka,Werema na Chenge wanachota 1.6 billion za umma kila mmoja na kudeposit kwenye akaunti zao binafsi unategemea wabongo wengine 48 millioni people watapataje mzunguko wa pesa walizochukua.

Kwa kutumia akili ndogo tu ya kukaa kijiweni kwa kukosa ajira unaweza kujiuliza kama genge lina watu lukuki walio ofisini na walistaafu na wote kwa miaka hamsini ya umaskini bongo wanaula bata Masaki kwa kutumia mabilioni ya pesa za umma sasa unadhani dawa zitatoka wapi hospitalini na unategemea wengine watapata wapi hela ya kula? na unategemea pesa za kuwezesha elimu bure zitatoka wapi? 

Hawa watoto wa mbwa tuliowanyima elimu bora technically watakosa na ajira na sasa ndo hao wanaturudi mchana kweupe! hawana cha kupoteza manake wana njaa na hawana namna ya kupata chakula kihalali! kwa mawazo yangu sera za magamba zimeshindwa kufanya kazi! nafikiri huu ni wakati watanzania wanatakiwa wasifanye kosa uchaguzi mkuu ujao, tujaribu na wengine hawa wameshindwa kwa miaka hamsini! inatosha!

Nyerere alisema nchi ina maadui watatu, ujinga , maradhi na umaskini, na sasa maadui badala ya kupungua wameongezeka, adui wa nne ni ufisadi! watanzania tuamke tuseme imetosha. nitafurahi watanzania wenzangu tukijaribu wengine! magamba wameiba sana na walifikiri hakuna kitakachotokea na sasa wanajionea kwa macho matokeo ya wizi wao kwa kuzalisha watoto hawa wa mbwa! 

Haya sasa na tuwapige mabomu na tuwafunge watoto wetu wenyewe tuliowanyima elimu na ajira kwa kuiba mali zao za umma kwa miaka hamsini ya umaskini! ninaamini safari ni ndefu , kwa tathmini zangu ndogo za sosiolojia ya Mlimani bomu ni kubwa sana hapa bongo kuliko tunavyodhani na sio kwamba ninaombea itokee ila kimantiki na tutegemee makubwa zaidi ya sasa ya watoto wa mbwa kama social and economic conditions za bongo hazitachange hasa this unequal distribution of resources iliyokithiri bongo manake gap la walio nacho na masikini ni kubwa sana kwa sasa! hebu angalia mtu ana 1.6b na mwingine hana 200 ya kunywa chai asubuhi! 

Nadhani kama hatutadeal na current situation kwa namna inavyopasa na si kinafiki na kwa jazba basi huko tuendako tutahitaji wanajeshi kabisa kuingia vitani kushughulikia na kudhibiti watoto na vijana wasio na elimu na ajira! ni mtazamo tu!

No comments:

Post a Comment