Januari:
Uandikishaji wapiga kura- Mwishoni
mwa mwezi huu uandikishaji upya wa wapigakura utaanza nchi nzima, mchakato
ambao utasimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Februari:
Uamuzi mgumu CCM- Chama
cha Mapinduzi (CCM), kiitatoa uamuzi kuhusu wanachama wake waliotiwa hatiani
kwa kufanya kampeni mapema na vitendo vilivyokiuka maadili ndani ya chama na
ndani ya jamii.
Machi:
BRT kukamilika- Mradi wa
ujenzi wa barabara ya mabasi ya endayo haraka (BRT) kuanzia Kimara hadi Posta
na Moroco-Magomeni utakamilika chini ya Mkandarasi Strabag International kutoka
Ujerumani na Mhandisi Msimamizi SMEC International ya Australia.
Aprili:
Kura za maoni- Aprili 30
itakuwa ndiyo siku ya upigaji wa kura za maoni za ama kupitisha au kuikataa
Katiba Inayopendekezwa kama ilivyotangazwa na Rais Jakaya Kikwete.
Mei:
CCM vs Ukawa- Vyama vya siasa
vinatarajiwa kuanza kuteua wagombea wa nafasi za urais na hapa ndipo mchuano
kamili kati ya CCM na Ukawa unatarajiwa kuanza rasmi.
Juni:
Bajeti ya kwanza- Mkutano wa
Bunge la Bajeti utapitisha Bajeti ambayo sehemu yake itatumiwa na Serikali ya
awamu ya tano, hivyo itatoa taswira ya uchumi wa Serikali ijayo chini ya rais
mpya baada ya Jakaya Kikwete kumaliza ngwe yake
Julai:
Bunge kuvunjwa- Mkutano wa 20
wa Bunge utakamilika na Bunge litavunjwa na Rais Kikwete, ikiwa ni ishara ya
kupuliza kipenga cha wabunge na wananchi wengine kuanza mbio kuelekea kwenye
uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani.
Agosti:
Kampeni kuanza-Ni mwezi
ambao zitaanza rasmi kampeni za uchaguzi mkuu, kwa vyama vyote vya siasa
vitakavyoshiriki uchaguzi mkuu kuaomba ridhaa ya wananchi kwa kunadi sera zao
ili vipate fursa ya kuwaongoza.
Septemba:
Ligi Kuu Bara- Msimu
mwingine wa Ligi Kuu ya Vodacom utaanza ambapo timu kadhaa zitashiriki ligi
hiyo inayaotarajiwa kuwa na mikikimikiki , ligi inayoendelea ilikuwa imejaa
matukio mengi yakiwamo ya kufukuza makocha.
Oktoba:
Rais Mpya- Utafanyika
Uchaguzi Mkuu wa kumpata rais mpya atakayeongoza Tanzania hadi 2020. Vyama
zaidi ya 20 vya siasa vinatarajia kusimamisha wagombea katika nafasi
mbalimbali.
Novemba:
Rais kuapishwa- Matokeo ya
uchaguzi Mkuu yatakamilika na Jaji Mkuu atamwapisha Rais mpya kushika madaraka
hayo ya juu nchini. Shughuli hiyo inatarajiwa kufanyika mbele ya viongozi
mbalimbali maarufu wa ndani na nje ya nchi. Baada ya hatua hiyo Rais Kikwete
ataingia rasmi kwenye orodha ya marais wastaafu.
Desemba: Sherehe za uhuru- Rais mpya
atapata fursa ya kukagua gwaride la kwanza la miaka 54 ya Uhuru, ikiwa ndio
sherehe yake ya kwanza ya kitaifa tangu kuapishwa kwake.
No comments:
Post a Comment