
Tanzania itachagua timu ya taifa ya mpira wa wavu mwishoni mwa mwezi huu kwa ajili ya michuano ya ufukweni ya Kanda ya 5 Afrika itakayofanyika kati kati ya mwezi Februari.
Timu itakayochaguliwa itapambana na timu kutoka Kenya, Burundi, Somalia, Ethiopia, Djibouti and wenyeji Tanzania katika michuano hiyo itakayofanyika kwa siku mbili kuanzia FEbruari 16.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuwa wenyeji wa michuano hii mikubwa ya mpira wa ufukweni, ambao haujapata umaarufu sana nchini licha ya nchi kuwa na fukwe nyingi zenye mandhari ya kuvutia
“Tutafanya michuano ya wazi Januari 24 na kuchagua timu siku hiyo itakayopambana na timu pinzani kutoka nchi shiriki”, amesema mkurugenzi wa kamisheni ya mpira wa ufukweni Tanzania, Muharrami Mchume.
Michuano hiyo itakuwa ni sehemu ya kufuzu kucheza michuano ya Olimpiki itakayofanyika mwakani Rio de Janeiro, nchini Brazil.
Kenya na Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika ya Mashariki zilizochaguliwa na shirikisho la mpira wa wavu Afrika (CAVB) kuwa wenyeji wa miongoni mwa michuano ya kufuku kucheza Olimpiki katika mpira wa wavu.
No comments:
Post a Comment