Wakati nikiwa kwenye gari asubuh ya nilikuwa ninasikiliza Radio ya Clouds FM na kwenye moja ya segment zao mwenyekiti wa bodi ya TANESCO (Robert Mbona) alisema kuwa ifikapo Marchi mwakani issue ya mgao wa umeme nchini itabaki historia. Kwa kuwa TANESCO imejipanga kuboresha miundo mbinu yake ya sasa kuweka kukidhi mahitaji ya wananchi wengi na pia shirika hilo kujiendesha kwa faida. Kwa kuwa pindi baada ya kuboresha miundo mbinu yao wana lengo la kupunguza utegemezi wao kwa makampuni binafsi yanayozalisha umeme na kuwauzia wao. Hivyo shirika litaweza kupata faida na kupeleka gawio kwa serikali.
Je, kwa hali ilivyo sasa huyu mtu ni wa kuaminika kweli baada ya kuwa mmoja kati ya watuhumiwa wa ile kamati ya bunge ya PAC?
Mara zote serikali ya CCM imekuwa ikipewa kashfa kuwa mara zote wamekuwa wakitumia mgongo wa TANESCO kuweza kupata pesa za kuiwezesha kugharamia uchaguzi wa chama chao. Je, kama anayosema mmoja wa watuhumiwa wa wizi wa account ya ESCROW kwa mujibu wa ripoti ya PAC ikiwa kweli. Je, CCM imeshapata chanzo chake kipya cha kupatia fedha halali ambacho hakitatuumiza tena watanzania.
Mie sijui tujuzane katika hili.
Source: Clouds FM
No comments:
Post a Comment