Ndiyo unampenda na yeye pia anakupenda ila ili upendo uweze kuendelea kudumu ni vizuri kujitahidi na kuwa tofauti kulinganisha na wale EX wake wa mwanzoni.. Utofauti huo unatakiwa uwe kwenye mambo tofauti kama tabia, ushirikiano, kusikilizana pamoja na zawadi mpeanazo.
Mpenzi yeyote mwema uthamini zawadi ya mpenzio pasipo kuangalia thamani yake.. Maana tu ile hali ya mtu kuona umuhimu wa kukuzawadia tu kitu ni tunu tosha moyoni kwa mpenzie. Hivyo ili wapenzi wetu watuthamini na kutujali ni vizuri kujitahidi na kutoa zawadi za kipekee ili zawadi hiyo iweke kuwa kumbukumbu nzuri kwa mpenzi kwa muda mrefu.

No comments:
Post a Comment